Uhamisho wa mifugo Samburu kila msimu

  • | Citizen TV
    192 views

    Swala la uhaba wa malisho ya mifugo, limezikosesha jamii za wafugaji amani huku baadhi wakizozana hadi kusababisha maafa. Katika kaunti ya Samburu, jamii hiyo imegeukia mbinu za zamani za kutenga sehemu za malisho ambapo mifugo hawaruhusiwi kulishwa hadi wakati wa ukame. Sehemu moja ikiisha nyasi, basi mifugo huhamishiwa sehemu nyingine iliyotengwa na kuzingirwa kwa ua.