Uhifadhi wa Afrika wajadiliwa Kigali, Rwanda

  • | VOA Swahili
    1,555 views
    Kuna haja ya haraka kwa nchi za Afrika kuongeza kiwango cha uwekezaji katika uhifadhi wa bioanuwai na huduma za mfumo wa ikolojia. Katika mkutano uanendelea mjini Kigali Rwanda, afrika ina pengo la dola million 7 ilikufikia azma yake ya kujitegema kama bara katika uhifadhi. Na kama anavyoripoti Hubbah Abdi akiwa Kigali Rwanda viongozi wa afrika wamehimizwa kujiunga na mkataba huo na kufanya juhudi za afrika kuwa endelevu. ##### Wakenya wanapokaribia kupiga kura agosti 9 mwaka huu , kampuni ya Usiku Games imezindua mchezo wa elimu ya uraia ili kuwawezesha wapiga kura kwa mara ya kwanza nchini Kenya kufanya maamuzi sahihi kuhusu viongozi watakaowachagua katika uchaguzi ujao. Mchezo huo mpya unaopewa jina la WEWE, unalenga kuwafundisha vijana kuwa na fikra makini na kupiga kura kwa kuzingatia sifa si makabila. Hubbah Abdi anarifu zaidi. ##### Huku mzozo wa chakula ukiubuka duniani kote kama athari za uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, Rais wa Russia Vladimir Putin alikutana na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mji mkuu wa Iran, Tehran, wakiangazia macho yao kufikia makubaliano ya kuanzisha usafirishaji wa nafaka ya Ukraine kupitia bahari nyeusi. Sunday Shomari ana taarifa zaidi.