Uhuru: Ajenda yangu mwaka huu ni kupunguza cheche za siasa

  • | Citizen TV
    Mabadiliko aliyofanya Rais Uhuru Kenyatta katika baraza la mawaziri na maagizo ya mpangilio wa kazi yanalenga kujibu madai ya wakosoaji wake kuwa amepoteza ramani ya uongozi na kutekwa nyara na siasa za kumrithi katika uchaguzi wa 2022. Kulingana na rais, ajenda yake kuu mwaka huu ni kupunguza cheche za siasa na kulenga masuala ya kuimarisha uchumi wa taifa.