Uingereza kusaidia Kenya katika vita dhidi ya COVID – 19

  • | Citizen TV
    Waziri wa masuala ya kigeni kutoka Uingereza Dominic Raab anasema serikali ya uingereza inazidisha ushirikiano na Kenya katika kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona hapa nchini. Japo Raab hajatoa maelezo kuhusu mpango huo, anatarajiwa kuandaa majadiliano na waziri wa afya Mutahi Kagwe ambapo makubaliano zaidi yataafikiwa. Raab amezungumza alipoandamana na waziri wa masuala ya kigeni nchini Balozi Raychelle Omamo ambaye ameeleza ushirikiano zaidi utajiri kuhusu masuala ya usalama afya na mabadiliko ya hali ya anga.