Uingereza yaeleza hatua ya suluhisho la Kuwepo Mataifa mawili

  • | VOA Swahili
    409 views
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron aliwasili Jumatano katika ghala la polisi mpakani Bulgaria karibu na Uwanja wa Ndege wa Sofia, ambako polisi wa Bulgaria wanahifadhi maboti yaliokusudiwa kutumika katika uvukaji mpaka haramu kupitia lango la English Channel ambapo polisi wa Bulgaria waliyakamata kwa msaada wa Uingereza.⁣ Akijibu swali kuhusu suluhisho la mataifa mawili huko Mashariki ya Kati alisema: “Sawa kile ambacho siku zote tumesema ni kuwa tunaunga mkono suluhisho la kuundwa mataifa mawili. Tunataka kuwepo Israel iliyo salama, huku ikiwepo Palestina iliyokuwa salama. Hii ndiyo njia ya kuwapa matumaini na heshima na amani, upande wa Waisraeli na Wapalestina. Sasa bila shaka, iwapo utakuwa na suluhisho la mataifa mawili, katika hatua fulani, itabidi uitambue Palestina kuwa ni taifa. Na kile nilichosema ni kuwa haihitajiki kusubiri mpaka mchakato huo ukamilike. Usianze katika hatua za mwanzoni kwa sababu Wapalestina wanahitajika kufanya mageuzi na mabadiliko, kwa uchache wake ni katika mamlaka za Palestina, lakini inaweza kuja kama ni sehemu ya mchakato huo. Nafikiri hiyo ndiyo njia iliyosawa.” - Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran #davidcameron #bulgaria ⁣