Ujangili North Rift I Kaunti ndogo tatu kubuniwa katika kaunti ta Turkana

  • | KBC Video
    32 views

    Kaunti ndogo tatu zitabuniwa katika kaunti ta Turkana kuimarisha juhudi za kukabiliana na tatizo la kudorora kwa usalama eneo hilo. Waziri wa usalama wa taifa Kithure Kindiki ameyasema hayo alipozuru eneo la Lokori kwenye eneo bunge la Turkana mashariki. Kindiki amesema serikali itabuni Kaunti ndogo za Lokiriama , Aroo na Siguta ili kuimarisha usalama. Kindiki pia ametangaza kwamba serikali itatumia shilingi milioni 100 kujenga shule zilizoharibiwa na majangili eneo hilo. Idadi ya maafisa wa polisi wa ziada na kitengo cha kuzuia wizi wa mifugo pia itaongezwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #darubini