- 17,353 viewsDuration: 1:19Mashirika ya msaada yanatahadharisha ukame wa muda mrefu umesababisha uhaba mkubwa wa chakula katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Kenya, Somalia, Ethiopia. Nchini Kenya kwa mfano, serikali imesema zaidi ya watu milioni 3 wanakabiliwa na njaa ya kiwango cha juu, hasa katika kaunti za Kaskazini mwa nchi hiyo. Uhaba huu wa chakula umewaathiri zaidi Watoto na watu wazima, pamoja na mamia ya mifugo ambayo imekufa kwa kukosa maji na malishi ya kutosha. Mwandishi wa BBC Sammy Awami alitembelea kaunti ya Turkana, moja ya zilizoathirika na ukame, na kutuandalia taarifa ifuatayo. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw