Ukanda wa Gaza: Familia ya Kipalestina inaeleza dhiki inayowakabili wakiwa na mtoto mchanga

  • | VOA Swahili
    278 views
    Wakiwa wamelazimika kukimbia makazi yao, kutokana na vita kati ya Israel na Hamas, Israa al-Jumalah na familia yake wamekuwa wanaishi katika mahema ya muda katika viwanja vya hospitali ya Shuhada al-Aqsa huko mji wa Deir al-Balah. Familia inahangaika kutafuta maziwa na mavazi ya mtoto wao, ikimlazimu mama yake kumlaza mwanawe aliyepewa jina la Israa kulala katika godoro sakafuni kwenye makazi yaliyotengenezwa kwa mbao. Israa anaeleza kuwa: “Tunakabiliwa na hali ngumu sana, tunaishi katika hema tukikosa mahitaji muhimu, na kwenye baridi, wakati wa baridi, hali ya hewa iliyopo hivi sasa, binti yangu anahitaji vitu vingi – maziwa, diapers, kwa kuwa mama yake, maziwa yangu hayatoshi kumnyonyesha, kama mtoto anahitaji vitu venye virutubisho, maziwa ya kumfanya akuwe.” - Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #hospitali #Nasser #wagonjwa #madawa