UKUMBI WA FREEMASON WAFUNGWA KWA KUTOLIPA KODI YA SHILINGI MILIONI 19

  • | K24 Video
    3,099 views

    Idara ya Mapato ya Kaunti ya Nairobi imefunga Ukumbi wa Freemason unaomilikiwa na Grand Lodge of East Africa katikati ya jiji kwa madai ya kutolipa ada ya ardhi ya shilingi milioni 19. Operesheni hiyo iliongozwa na Waziri wa Afya wa Kaunti Suzanne Silantoi na Afisa Mkuu wa Nyumba Lydia Mathia, kama sehemu ya kampeni ya kuwakabili wadaiwa sugu wa ushuru jijini.