UNHCR yaitaka Uganda kuchunguza mauaji ya wakimbizi 10 : AMKA NA BBC 18 09 2020

  • | BBC Swahili
    Katika Amka na BBC, Kimbunga Sally kilichokumba baadhi ya maeneo ya Marekani kinazidi kuleta madhara baada kuendelea kwa mvua nyingi na mafuriko katika majimbo ya Carolina na Georgia. Shirika la umoja mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Uganda kuchunguza mauaji ya wakimbizi 10 yaliyofanyika katika kambi ya Rhino Kaskazini mwa nchi mwishoni mwa wiki. Wakati dunia ikiendelea kupambana na janga la virus vya Corona,bado kuna hofu kwamba huenda visa vya maambukizi vikaongezeka zaidi , kwa sasa duniani kote watalaam wanaendelea kuumiza vichwa ili kupata tiba ya Virusi hivyo vilivyoitikisa ulimwenguni kote. Usikose kuungana nasi muda ukiwadia ukiwa na Leonard Mubali na David Nkya akiunguruma michezoni.