Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine wafariki katika ajali ya helikopta

  • | BBC Swahili
    1,014 views
    Watu watatu wakuu katika wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine wameuawa katika ajali ya helikopta kando ya kitalu katika kitongoji cha mashariki mwa mji mkuu Kyiv. Waziri wa Mambo ya Ndani Denys Monastyrsky, 42, alikufa pamoja na naibu wake wa kwanza wa waziri na katibu wa serikali. Watu 16 walikufa wakati helikopta hiyo ilipoanguka huko Brovary, wakiwemo watoto watatu, kulingana na maelezo yaliyosasishwa kutoka kwa rais wa Ukraine. Bw Monastyrsky ndiye muathirika wa juu zaidi wa Ukraine tangu vita kuanza. #bbcswahili #Ukraine #Kyiv