Upandikizaji wa konea wafanikishwa katika hospitali ya Moi Eldoret

  • | K24 Video
    354 views

    Licha ya kuwepo kwa utashi wa viungo muhimu vya binadamu nchini, Kenya bado haijaridhia swala la watu kutoa viungo vyao kutumika baada ya kuaga dunia. Katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya moi zaidi ya wagonjwa mia tatu wa macho wanahitaji konea. Ukosefu wa konea unamaanisha huenda wasipate uwezo wa kuona ila kwa wenye uwezo watalazimika kununua kutoka taifa la Marekani ambako watu hutoa konea zao kutumika tena wakishaaga dunia. Mahojiano na daktari mkuu wa macho katika hospitali ya Moi anayesema wakati umefika wakenya kuiga mfano wa marekani wa kusaidia wagonjwa. je inawezekana?