Skip to main content
Skip to main content

Upinzani wapinga ujenzi wa kituo cha Ebola Laikipia

  • | Citizen TV
    91 views
    Viongozi wa upinzani wameendelea kupinga ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola kwa raia wa Marekani katika kaunti ya Laikipia. Kinara wa chama cha PLP Martha Karua na katibu mkuu wa chama cha DCP John Methu wamemtaka Rais William Ruto kusikiliza pingamizi za Wakenya kuhusu swala hilo. Wakizungumza katika hafla tofauti katika kaunti za Kirinyaga na Nairobi, viongozi hao waliunga mkono maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika mjini Nanyuki wakitaka Wakenya kuendelea kutetea haki na usalama wao.