Ureno: Moto waharibu maelfu ya hekta za ardhi, msitu, na eneo la utalii

  • | VOA Swahili
    72 views
    Mamia ya wafanyakazi wa idara ya zima moto wamekuwa wakipambana na moto wa msituni unaoendelea kuwaka kusini mwa Ureno ambao tayari umetekekeza maelfu ya hekta za ardhi na kuwalazimsha watu 1 400 kuondoka katika makazi yao ikiwa ni hatua ya tahadhari. Wazima moto elfu 8 kwa hivi sasa wanapambana na moto huo wa msituni ulioanza Agosti 5 katika tarafa ya Odemira kwenye jimbo la Alentejo. Lakini tangu kuanza kuwaka umeshaenea kusini kuelekea Algarve moja ya vivutio vya utalii nchini Ureno. Joto kali na upepo umesababisha hali kuwa ngumu kupambana na moto ambao umeshaharibu hekta 6 700 za msitu. Mataifa ya kusini mwa Ulaya kama Ureno yamekabiliwa na hali mbaya ya moto wa msitu kutokana hasa na hali ya joto ambayo haijawahi kushuhudiwa wakati wa kilele cha msimu wa utali, na kuwasababisha maafisa kutoa tahadhari ya afya. #moto #wazimamoto #idara #misitu #uharibifu #ardhi #ureno #utalii #joto #voa #voaswahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.