Urusi-Ukraine : Mtoto afanyiwa upasuaji gizani baada ya makombora kurushwa Kyiv

  • | BBC Swahili
    544 views
    Mnamo tarehe 23 Novemba, wakati makombora ya Urusi yalipopiga mji mkuu wa Ukraine, Taasisi ya Moyo ya Kyiv iliachwa bila umeme. Timu ya madaktari iliendelea kufanya kazi licha ya kukatikakwa umeme; kumfanyia mtoto upasuaji wa moyo chini ya mwanga hafifu wa tochi za LED za mkononi na usaidizi fulani kutoka kwa jenereta. Wakati wa siku ya shambulio hilo, hospitali ilifanikiwa kukamilisha upasuaji 10 wa kufungua moyo. BBC ilizungumza na Profesa Borys Todurov, ambaye anaongoza timu hizo zilipokuwa zikifanya kazi karibu na giza. #ukraine #bbcswahili #afya