Usalama Mahakamani I Mahakama yasitisha shughuli kwenye majengo ya muda

  • | KBC Video
    16 views

    Idara ya mahakama imesimamisha utatuzi wa kesi kwenye majengo ya muda kote nchini. Kupitia taarifa kutoka afisi ya jaji mkuu, idara ya mahakama imesema haitahatarisha maisha ya maafisa wake na itadumisha usalama wao hasa katika maeneo ambako miundo msingi ni duni. Kesho Jumanne tarehe 18 imetengwa kuwa siku ya maombolezo kukumbuka hakimu mkuu Monicah Kivuti ambaye alipigwa risasi akiwa kazini. Vikao vya mahakama kote nchini vitarejelewa Jumatano isipokuwa mahakama ya Makadara ambayo inachunguzwa upya kwa sababu za kiusalama.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive