Usalama waimarishwa katika kaunti ya Lamu baada ya shambulizi la punde

  • | Citizen TV
    176 views

    Usalama umeimarishwa kaunti ya Lamu, baada ya shambulizi la punde kuwaua watu watano katika kijiji cha Salama-Kibaoni wadi ya Mkunumbi. Gavana wa Lamu Issa Timamy na maafisa wakuu wa usalama wanazuru kijiji hiki kutathmini hali na kuwasaidia waathiriwa, ambao nyumba zao ziliteketezwa na magaidi walioshambulia kijiji hicho. Wanamgambo walivamia kijiji hiki usiku wa kuamkia jumapili, huku hali ikiendelea kusalia tete katika eneo hili. Shambulizi hili ni la pili kushuhudiwa Lamu katika muda wa chini ya juma moja.