USALAMA WAIMARISHWA KWENYE BUNGE LA MAREKANI KUELEKEA KUAPISHWA KWA JOE BIDEN

  • | VOA Swahili
    Hali ya usalama imeimarishwa kuliko ilivyo kawaida katika mji mkuu wa washington DC, wiki moja kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden, Januari 20. Maafisa wa usalama, wameshika doria kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa, ili kuepusha vurugu kama ilivyotokea Januari 6 pale maelfu ya wafuasi wa Rais Donald Trump walipovamia majengo ya bunge la Marekani.