Ushahidi watolewa kuhusu mauaji ya Edwin Chiloba

  • | Citizen TV
    424 views

    Wavulana wawili akiwemo binamu wa mshukiwa mkuu katika mauaji ya mwanamitindo na mtetezi wa watu wa jinsia moja Edwin Chiloba wameambia mahakama kwamba walimsaidia mshukiwa Jackton Odhimbo kubeba sanduku la chuma ambalo lilikuwa na mwili wa Chiloba.Walipokuwa wakitoa ushahidi wakati wa kusikizwa kwa kesi mbele ya Jaji Reuben Nyakundi katika Mahakama Kuu mjini Eldoret, wawili hao wenye umri wa miaka 17 waliieleza mahakama kuwa walimsaidia Odhiambo kupakia sanduku kwenye gari mnamo Januari 3.Hata hivyo, mashahidi hao walikiri kuwa hawakufungua kisanduku hicho na wala hawakujua kilichomo ndani yake hadi siku kadhaa baadae walipohojiwa na maafisa wa DCI na kuonyeshwa picha za mwili wa marehemu Chiloba kwenye sanduku hilo .