Ushuru zaidi kwa wakenya watajwa kama mzigo mzito

  • | Citizen TV
    2,561 views

    Wanauchumi kutoka taasisi ya maswala ya uchumi, kampuni ya price water house coopers na muungano wa benki nchini ni miongoni wamepinga baadhi ya vipengee kwenye mswada wa fedha wa mwaka 2023 na kusema kuwa vinakwenda kinyume na katiba. Wakiwasilisha maoni yao mbele ya kamati ya fedha, wadau hao wamepinga mapendekezo ya kuwatoza wakenya ushuru zaidi na kusema gharama ya maisha itapanda maradufu.