Utamaduni wa Wateso kutoka Busia

  • | Citizen TV
    390 views

    Jamii ya Iteso inaopatikana Magharibi mwa Kenya na Mashariki mwa taifa jirani la Uganda ni mojawapo ya jamii ambazo bado zinafuata kwa makini mila na desturi zao. Teso ni mojawapo ya jamii zenye idadi ndogo ya watu nchini Kenya walioaminika kuhamia nchini kutoka Uganda na wanaopatikana kwa wingi katika kaunti ya mpakani ya Busia. Ni jamii yenye mila na desturi zinazofanana sana na za wenzao wa Uganda.