- 10,708 viewsDuration: 3:29Utata wa shule ya wasichana ya St Mary's Lwak huko Siaya kuhusu mwanafunzi aliyeondolewa shuleni kwa sababu ya kuvaa Hijab umefika bungeni leo huku sasa wizara ya elimu ikiagizwa mwanafunzi huyo kurejeshwa shuleni mara moja. Katibu wa elimu Julius Bitok amejipata lawamani alipofika mbele ya kamati ya uhasibu kuzungumzia mgao wa shule. Aidha, Waziri wa afya Aden Duale akiungana na viongozi wengine kukashifu kisa cha binti kukatazwa kuvaa hijab shuleni kuambatana na dini ya kiisilamu kuwa ubaguzi