Uzinduzi wa DCP wakumbwa na Rabsha na vurugu huku wanahabari wakijeruhiwa na vifaa vyao kuharibiwa

  • | Citizen TV
    5,368 views

    Rabsha na Vurugu zilishuhudiwa katika uzinduzi wa chama cha Democracy for the Citizens Party DCP kinachoongozwa na Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, baada ya kundi la vijana kuvuruga mkutano huo. Watu kadhaa wakiwemo wanahabari watatu walijeruhiwa huku walinzi wa Gachagua wakiwalazimisha wanahabari kufuta kanda za video walizorekodi kufuatia vurugu hizo na vifaa vyao vya kazi vikichukuliwa kwa muda.