Vifo vinavyotokana na mafuriko vyaongezeka

  • | K24 Video
    693 views

    Idadi ya watu waliokufa maji baada ya lori kusombwa na maji katika mto Muswii eneo la Sultan kaunti ya Makueni imefika tisa. Hii ni baada ya miili mingine minne kuopolewa leo huku wengine kumi wakiwa hawajulikani waliko, na katika kaunti ya Machakos watu wanne wameripotiwa kufa maji usiku wa kuamkia leo baada ya gari lao kusombwa na maji wakivuka mto manyanzani eneo la Yaitha kaunti ndogo ya Kalama.