VIFO VYA COVID 19 VYAONGEZEKA TANZANIA

  • | VOA Swahili
    Jumuiya ya kimataifa imeshtushwa na idadi ya vifo vinavyoendelea kutokea nchini Tanzania vikisemekana kusababishwa na Covid 19. Serikali ya Tanzania haisemi waziwazi kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo nchini na hakuna maelezo ya kina kuhusu juhudi zipi zinachukuliwa na mamlaka husika kukabiliana na janga la Covid 19 ikiwa ni pamoja na mpango wa nchi hiyo kupokea chanjo. #VOA #DL