- 665 viewsDuration: 3:26Familia moja kutoka kaunti ya machakos kaunti ndogo ya matungulu inalilia haki baada ya mwana wao wa gredi ya 10 kufariki shuleni. Mwanafunzi huyo alibanwa na lori la shule ukutani alipokuwa akisaidia kulikwamua. Haya ni huku upasuaji wa mwili wa mwanafunzi wa gredi 8 wa shule ya msingi ya moi ambaye alifariki jana shuleni , ukibaini kuwa alifariki kutokana na matatizo ya kupumua.