Vifo zaidi Binzaro: Watoto 6 wa Otieno Wafariki

  • | Citizen TV
    1,813 views

    Familia ya Jarius Otieno aliyendamana na watoto wake sita imethibitisha kuwa watoto hao waliangamia katika kijiji cha kwa binzaro kaunti ya kilifi. Familia hiyo inadai kuwa Otieno na mkewe walikiri kufariki kwa wana wao na kudokeza kuwa makumi ya wafuasi wa dhehebu hilo potovu wamefariki tangu mwezi machi. Inadaiwa kuwa mhubiri tata Paul Mackenzie amekuwa akiwasiliana na wafuasi hao kwa njia ya simu akiwa kizuizini.