Vijana wa Kimarekani wageukia wabunifu wa Kiafrika kutengeneza magauni

  • | BBC Swahili
    686 views
    Vijana wa Kimarekani sasa wanawageukia wabunifu wa Kiafrika kutengeneza magauni yao ya ndoto kwa ajili ya prom. Ingawa prom siyo desturi barani Afrika, wabunifu watano wamesema wametuma karibu magauni 3,000 nchini Marekani mwaka huu pekee. BBC imezungumza na baadhi ya wasichana wa Kimarekani wanaosema walijihisi kama princessi na malkia wa Kiafrika. Kwa wabunifu, hii ni fursa ya kusafirisha ubunifu na mtindo wa Kiafrika, huku wakifungua masoko mapya. Habari ya Mwandishi wa BBC Chiamaka Enendu inasimuliwa na @frankmavura. #bbcswahili #africanpromdress #tanzaniatiktok Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw