Vijana wapinga kunyanyaswa na polisi kwa madai ya uhalifu

  • | Citizen TV
    731 views

    Mzozo umeibuka kati ya polisi na vijana wanaojitafutia riziki katika jaa la mji wa Nanyuki huku polisi wakiwafurusha vijana hao kwa madai kwamba wamekuwa wakitekeleza uhalifu na kukimbilia eneo hili. Vijana hao ambao ni zaidi ya 200, wanasema wanafanya biashara halali. Vijana hao hukusanya plastiki na chupa na kutumia pesa wanazopata kufuga nguruwe na sungura.