Skip to main content
Skip to main content

Vijana waraiwa kujiunga na taasisi za kiufundi mashinani huko Malindi

  • | Citizen TV
    35 views
    Wito umetolewa kwa vijana kujiunga na taasisi za kiufundi mashinani ili kupata ujuzi wa kuwawezesha kujiajiri au kupata nafasi za ajira katika sekta ya Uchumi wa baharini. Katika kaunti ya Kilifi, Zaidi ya vijana laki tatu hawana ujuzi wa kuwawezesha kupata fursa katika soko la ajira.Wakizungumza katika taasisi ya kiufundi ya Muyeye eneo bunge la Malindi, wadau waliwahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kuchukua fursa zilizoko kwenye vyuo vya mafunzo ya uchumi wa majini.