Vijana watano waliotekwa nyara waachiliwa na kurejea kwa familia zao

  • | Citizen TV
    15,241 views

    Familia za vijana watano kati ya sita waliotekwa nyara kwa zaidi ya wiki mbili sasa zimeshusha pumzi baada ya vijana hao kuachiliwa Billy Mwangi, Peter Muteti, Bernard Kavuli na, Kibet Bull na Rony Kiplangat wameachiliwa huru na kuungana na familia zao. Waliotekwa hawajasimulia yaliyojiri na wanaonekana kuchanganyikiwa. Mmoja miongoni mwa waliotekwa nyara, Steve Mbisi bado hajulikani aliko hadi sasa.