Skip to main content
Skip to main content

Vijana wavamia mochari Nairobi, wachukua jeneza la rafiki aliyefariki kwa mafuriko

  • | Citizen TV
    24,745 views
    Duration: 3:16
    Kizaazaa kimeshuhudiwa leo katika makafani ya Nairobi baada ya kundi la vijana kufika na kutwaa kwa nguvu mwili wa rafiki yao. Vijana hao waliingia kwa nguvu ndani ya mochari na kuchukua jeneza la marehemu nicholas kyalo, aliyefariki kwa mafuriko ijumaa iliyopita. Hata hivyo, zogo lilizidi pale walipogundua kuwa sanduku halikuwa na mwili. Maiti zaidi za waathiriwa wa mafuriko zimefikishwa katika hifadhi na kufikisha 30 idadi ya waliofariki Nairobi.