Vikao vya uchunguzi wa mauaji ya Rex Masai vimeendelea leo mahakamani

  • | Citizen TV
    2,088 views

    Vikao vya uchunguzi wa mauaji ya Rex Masai wakati wa maandamano ya Gen z ya Juni mwaka jana vimeendelea leo mahakamani, huku aliyekuwa kamanda wa polisi kituo cha Central jijini Nairobi, Dorris Mugambi akikana kuhusika kwa polisi wa kituo hicho katika mauaji ya kijana huyo. Ushahidi wa Mugambi umetolewa huku mashahidi wengine kumi wakitarajiwa kutoa ushahidi.