Vikosi vya Usalama vya Israeli vyawaokoa raia waliotekwa nyara na wanamgambo

  • | VOA Swahili
    829 views
    Polisi nchini Israeli imetoa mkanda wa video Jumapili ukionyesha vikosi vya usalama vikiwaokoa raia wakati wakitupiana risasi katika eneo linalojulikana kama Gaza envelop. Gaza envelop ni jina lililopewa maeneo yanayokaliwa kwa wingi na Waisraeli ambayo yako ndani ya kilomita 7 (maili 4.3 ya mpaka wa Ukingo wa Gaza. Mapigano yalikuwa yanaendelea upande wa Kusini mwa Israeli Jumapili kwa zaidi ya saa 24 baada ya kikundi cha wapiganaji wa Palestina kufanya uvamizi uliokuwa haujatarajiwa. Wapiganaji hao waliwachukua mateka wao katika eneo la pwani, wakiwemo wanawake, watoto, na watu wazima. #israel #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas