Viongozi Banisa, Mandera wakutana na kuhimiza jamii kudumisha utulivu

  • | KBC Video
    36 views

    Ghasia za kijamii zilizozuka katika kijiji kimoja nchini Ethiopia kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Kenya zilisambaa na kuathiri eneo la Banisa katika kaunti ya Mandera. Kufuatia ghasia hizo zilizosababisha maafa, viongozi wa kaunti ya Mandera waliandaa kikao na wakazi ambapo umuhimu wa kudumisha amani na uwiano ulikaririwa. Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Banisa Hesbon Kayesi, aliwahimiza wakazi kukumbatia utangamano na akawataka wazee wa jamii kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha utulivu unadumishwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive