Viongozi kutoka eneo la kaskazini wataka suala la ukame lipewe kipaumbele

  • | K24 Video
    81 views

    Viongozi kutoka eneo la kaskazini mwa nchi sasa wanataka suala la ukame lipewe kipaumbele bunge litakaporejelea vikao vyake. Viongozi hao ambao wameendelea kushinikiza ukame kutangazwa kuwa janga la kitaifa na serikali ya sasa, wanasema wakati umefika jamii ya kimataifa ishirikishwe katika tatizo hilo ambalo limewaacha mamilioni ya wakenya na mifugo kaskazini mwa nchi katika hatari ya maangamizi.