Viongozi Nyamira wahimiza uangalifu

  • | Citizen TV
    143 views

    Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Nyamira wanawashauri wakazi kuwa waangalifu wakati huu ambapo mafuriko yanashuhudiwa nchini ili kujiepusha na visa vya kusombwa na maji. Kwenye mazishi ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo kikuu cha Maasai Mara aliyesombwa na mafuriko Narok, viongozi hao walihimiza serikali kuendelea kuahirisha shughuli za masomo nchini hadi pale mafuriko yakatapokwisha. viongozi hao wamesema kuw ausalama wa wanafunzi, walimu na wafanyikazi shuleni ni muhimu zaidi na kuwa kuahirishwa kwa ufunguzi wa shule kutasaidia kuziia maafa yanayotokana na mafuriko. Esther Kerubo alisombwa na maji alipokuwa akivuka mto Inkare.