Viongozi Samburu walalama fedha za El-Nino hazijatolewa

  • | Citizen TV
    180 views

    Mbunge wa Samburu Mashariki Jackson Lekumontare, ametoa wito kwa serikali kutoa fedha zilizotengwa mafuriko yanayotokana na mvua ya El Nino ili kuwashughulikia waathiriwa. Mbunge huyo amesema kuwa familia zisizopungua mia mbili hamsini zimeathirika na mafuriko katika eneo la lerata samburu mashariki. Familia hizo zimeachwa bila makao, chakula na bidhaa muhimu.