Viongozi wa Afrika waahidi kuisaidia Somalia katika vita dhidi ya al-Shabab

  • | VOA Swahili
    377 views
    Viongozi wa Djibouti, Ethiopia, Kenya na Somalia walikutana Jumatano huko Mogadishu kujadili vita vinavyoendelea dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab. Mkutano huo wa usalama unaowakutanisha viongozi umefanyika wakati Somalia na washirika wake wakifanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao wa Kiislam. Somalia katika miaka iliyopita imepata ushindi mkubwa dhidi ya kikundi hicho, ambacho pia kimeongeza mashambulizi yake dhidi ya majeshi ya serikali. Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi zilizoko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugaidi, umejumuisha Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Djibouti Omar Guelleh, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na mwenyeji wa mkutano huo, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud. #somalia #ethiopia #djibouti #kenya #williamruto #omarguelleh #abiyahmed #hassansheikhmohamud #alshabab - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.