Viongozi wa Azimio walalamikia jinsi serikali inavyoshughulikia suala la gharama kubwa ya maisha

  • | K24 Video
    69 views

    Wanachama wa Kamwene Unity Forum, ambao na baadhi ya viongozi wa Azimio la Umoja kutoka Mlima Kenya, wamelalamikia jinsi serikali ya Kenya Kwanza inavyoshughulikia suala la gharama kubwa ya maisha. Viongozi hao, wakiongozwa na Martha Karua na katibu mkuu wa chama cha Jubilee, Jeremiah Kioni, wameishutumu serikali ya Kenya Kwanza kwa kutokuwa na nia thabiti ya kulipa kipaumbele suala hilo wanalosema linastahili kuwa moja ya ajenda kuu za mazungumzo ya Bomas