Viongozi wa dunia, Afrika wahudhuria kumbukumbu ya mauaji ya kimbari

  • | VOA Swahili
    154 views
    Rwanda inaadhimisha miaka 30 ya kipindi cha kutisha zaidi katika historia ya taifa hilo ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi walio wachache. Hadi leo hii, makaburi mapya ya halaiki bado yanagunduliwa kote nchini humo kwenye watu milioni 14, jambo ambalo ni ukumbusho wa kusikitisha wa ukubwa wa mauaji hayo. Rais wa Rwanda Paul Kagame ameongoza hafla ya kumbukumbu ya kusikitisha katika mji mkuu Kigali Jumapili katika maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari. Wageni kutoka nje ya nchi wakiwemo viongozi wa Afrika Kusini, Congo, Ethiopia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Tanzania, pia Rais wa Israel Isaac Herzog. Marais wa zamani wa Marekani na Ufaransa Bill Clinton na Nicolas Sarkozy walihudhuria pia. Kagame aliwasha mwenge wa ukumbusho na kuweka shada la maua eneo la viunga vya kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo zaidi ya watu 250,000 wanaaminika kuzikwa. - VOA, AP ⁣ #rwanda #hakizabinadamu #kigali #paulkagame #voaswahili #mauaji #kimbari #viongozi #africa #dunia