Viongozi wa Dunia waeleza hisia zao kuhusu vita vya Israeli na Gaza

  • | VOA Swahili
    394 views
    Marekani inasimama pamoja na Israeli, “Rais Biden alisema katika hotuba yake kupitia televisheni.⁣ ⁣ Israeli ina haki ya kujitetea dhidi “ya shambulizi la kinyama”, Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema Jumapili, baada ya kikundi cha wanamgambo wa Palestina Hamas kufanya shambulizi kubwa la kushtukiza.⁣ ⁣ Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, alisema: “Kuwanyima haki za msingi za watu wa Palestina, hususan ile ya kuwepo taifa huru na lenye kujitawala, ni sababu kuu ya mzozo wa kudumu kati ya Waisraeli na Wapaletina.”⁣ ⁣ Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumapili aliisihi Israei na Kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas “ kuunga mkono amani” na kujiepusha kuwadhuru raia.⁣ ⁣ Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alieleza kuunga mkono shambulizi hilo, akiliita ni “operesheni ya ufahari”.⁣ ⁣ Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen alisema: “Nina laani vikali shambulizi lililofanywa na magaidi wa Hamas dhidi ya Israel.⁣ ⁣ Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia ilisema: “Ufalme unatoa wito kusimamishwa haraka kusambaa kwa vita kati ya pande mbili, kuwalinda raia, na kujizuia”.⁣ #israel #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas