Viongozi wa kaunti ya Lamu wataka usalama kuimarishwa baada ya mauaji

  • | Citizen TV
    359 views

    Viongozi wakuu serikali ya kaunti ya Lamu wameshinikiza Idara ya usalama kuweka kambi ya maafisa wa usalama maeneo ambayo yameshuhudia mashambulizi ya kigaidi. Miongoni mwa maeneo haya ni vijiji vya Juhudi, Marafa, Widho na Salama. Viongozi hao wamelaani vikali shambulizi la kigaidi ambalo limetokea Kijijiji cha Salama siku mbili zilizopita na kusababisha mauaji ya watu watano na nyumba zikichomwa moto na mali kuporwa.