Viongozi wa Kenya Kwanza kutoka Kiambu wasifia vikao cha kuangazia makuzi ya uchumi

  • | KBC Video
    7 views

    Baadhi ya wanasiasa wanaoegema mrengo wa Kenya Kwanza katika kaunti ya Kiambu wamesifia maazimio ya kikao cha kuangazia makuzi ya uchumi kilichoandaliwa na naibu rais William Ruto katika eneo hilo hapo jana. Viongozi hao waliokuwa kwenye eneo la Limuru walisema mbinu za ufufuzi wa uchumi zilizopendekezwa na mrengo wa Kenya Kwanza zitasaidia kuinua maisha ya wakazi wa Kiambu pamoja na kuimarisha biashara baina ya kaunti za eneo la Mlima Kenya. Hapo jana, naibu rais aliongoza kikao cha kiuchumi katika eneo la Kiambu ambako aliahidi kupunguza gharama ya kuzaliwa maziwa, kahawa na majani chai pamoja na kufufua viwanda vilivuokwama katika eneo hilo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #ThisIsKBC #News