Viongozi wa Kenya Kwanza wakosoa vitisho vya Azimio

  • | Citizen TV
    5,151 views

    Viongozi wa Kenya Kwanza wameendelea kukosoa upinzani kwa mipango yake ya kutaka kukusanya saini kumbandua mamlakani Rais William Ruto. Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula na hata katibu wa UDA Cleopas Malala wamepuuza mipango hiyo wakisema haina misingi yoyote kisheria. Na kama Martin Munene anavyoarifu, malala sasa akitaka kinara wa Azimio Raila Odinga kukamatwa kwa kile anasema ni uhaini.