- 1,197 viewsDuration: 2:15Viongozi wa mrengo wa Kenya Kwanza katika Kaunti ya Trans Nzoia wametangaza mpango wa kuzunguka wadi zote 25 za kaunti hiyo kukusanya maoni ya wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayohitajika. Hatua hiyo inalenga kuandaa ajenda ya masuala ya kupewa kipaumbele kabla ya ziara ya William Ruto eneo hilo mwezi ujao. Wakizungumza katika wadi ya Sitatunga, viongozi hao wamesema kuwa ziara hiyo itatoa fursa kwa wakazi kueleza changamoto zao moja kwa moja na kupendekeza miradi ya maendeleo kama vile uboreshaji wa miundombinu, afya, elimu na kilimo. Aidha, wametumia nafasi hiyo kuwarai wakazi wa kaunti hiyo kushirikiana na uongozi wa sasa ili kuharakisha utekelezaji wa miradi itakaidhinishwa wakati wa ziara hiyo ya rais.