Viongozi wa Kenya Kwanza wataka maandamano kusitishwa

  • | Citizen TV
    1,294 views

    Viongozi wanaoegemea upande wa serikali wametoa wito kwa wakenya kukomesha maandamano, na kuunga mkono serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Akizungumza katika kaunti ya Kajiado, naibu rais Profesa Kithure Kindiki aliwataka wanaopinga serikali kutoa suluhu kwa madhila yanayowakumba wakenya badala ya kurusha cheche na kashfa za kila mara. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, Semi sawia zilisheheni katika maeneo mbali mbali ambapo viongozi wa mrengo wa serikali walifanya michango kwa makundi tofauti.