- 261 viewsDuration: 1:28Viongozi wa kidini kutoka kaunti ya Mombasa wamewataka wanasiasa nchini kukoma kutoa matamshi yatakaoleta uhasama baina ya wakenya wanapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao. Wakizungumza huko makande huko mombasa baada ya uzinduzi wa baraza la wanaume wa kanisa la AIPCA wameghadhabishwa na kupanda kwa joto la kisasa nchini na kuelezea hofu ya maendeleo kukwama. Aidha wamewataka wanasiasa kukoma kutumia sehemu za ibada kueneza siasa na hata kutoa matamshi ya uchochezi. Baraza hilo limesema kuwa litaanzisha mchakato wa kuelimisha wakenya kuhusu majukumu yao.