- 202 viewsDuration: 2:29Viongozi wa kidini kutoka kaunti za Kaskazini Mashariki na Tana River wametaja matumizi mabaya ya mitandao na ukosefu wa hamasisho miongoni mwa vijana kama chanzo cha kuongezeka kwa maambukizi mapya virusi vya HIV. Takwimu kutoka baraza la kitaifa la kudhibiti magonjwa na majanga NSDCC za mwaka 2024 zinaonyesha kuwa maambukizi mapya ya Hiv ya watu wazima na vijana wa kati ya miaka 15 hadi 24 zilifikia 39% katika eneo hilo. Kwenye mkutano wa ushirikiano baina ya NSDCC na baraza la SUPKEM viongozi wa kidini wametakiwa kutumia majukwaa ya misikiti kuwahimiza waumini wao kuchukua hatua za kuzuia maambukizi zaidi...