Viongozi wa kidini wataka mabishano ya kisiasa kusitishwa

  • | Citizen TV
    479 views

    Viongozi wa kidini wamewarai wanasiasa nchini kushirikiana na kuleta watu pamoja ili kuafikia maendeleo. Viongozi hawa wa ngazi tofauti za kidini wamesema haya wakati siasa kati ya viongozi nchini zimenoga wakinyosheana vidole za lawama na kushabuliana hadharani.Viongozi hao wamewakosoa wanasiasa kwa kuibua mihemko miongoni mwa wananchi na kuzidisha cheche za kisiasa zinazotatiza utangamano. wamewataka viongozi kuwafanyia wananchi kazi na kufanikisha miradi ya maendeleo badala ya siasa za kila mara.